Jumamosi 4 Julai 2026 - 14:20
Ujumbe wa Harakati ya Hashd al-Shaabi Wafika Tehran Kushiriki Hafla ya Kuaga Imam Shahidi Khamenei

Hawza / Ujumbe wa Harakati ya Hashd al-Shaabi ukiongozwa na Faleh al-Fayyadh umewasili jana Ijumaa mjini Tehran kwa ajili ya kushiriki katika hafla ya kuaga Imam Shahidi Sayyid Ali Khamenei.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, ujumbe wa Harakati ya Hashd al-Shaabi ukiongozwa na Faleh al-Fayyadh umefika jana Ijumaa mjini Tehran kwa ajili ya kushiriki katika hafla ya kuaga Imam Shahidi Sayyid Ali Khamenei.

Katika taarifa iliyotolewa na Harakati ya Hashd al-Shaabi imeelezwa kwamba: Ujumbe wa Harakati ya Hashd al-Shaabi, ukiongozwa na Mwenyekiti wa harakati hiyo, Faleh al-Fayyadh, ukiambatana na Mkuu wa Makao Makuu ya Jeshi, Abdulaziz al-Muhammadawi, pamoja na idadi ya makamanda na wakurugenzi wa harakati hiyo, umefika katika mji mkuu wa Iran, Tehran, ili kushiriki katika hafla ya kumuaga Kiongozi aliyefariki dunia, Imam Shahidi Sayyid Ali Khamenei.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa ushiriki wa ujumbe huo unafanyika katika mfumo wa kuhudhuria hafla rasmi ya kuaga inayofanyika katika mji mkuu wa Iran, Tehran, kwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na ujumbe rasmi kutoka ndani ya Iran na kutoka nchi nyingine.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha